Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.
The use of this website is subject to the following terms of use:
You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:
Utangulizi - Ripoti Ya Kikosi Kazi
1.1 Usuli
Tanzania ilitimiza miaka sitini (60) ya Uhuru wa Tanzania Bara, miaka hamsini na saba (57) ya Mapinduzi ya Zanzibar na miaka hamsini na saba (57) ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mwaka 2021. Katika kipindi hiki, nchi yetu imepitia katika awamu za uongozi na mifumo mbalimbali iliyokusudia kuimarisha uhuru, umoja, amani, utulivu, demokrasia na utawala bora. Ripoti hii inahusu juhudi zinazoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Sita za kuimarisha na kuboresha mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa na Utawala Bora.
Kabla ya uhuru, chama cha siasa Tanganyika African National Union (TANU) kilichoanzishwa mwaka 1954 kikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kiliongoza jitihada za kutafuta uhuru wa Tanganyika. Pamoja na TANU kulikuwepo na vyama vya siasa vingine vikiwemo, United Tanganyika Party (UTP) kilichoanzishwa mwaka 1956, African National Congress (ANC) kilichoanzishwa mwaka 1958 na All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) kilichoanzishwa mwaka 1959 kwa upande wa Tanganyika. Kwa upande wa Zanzibar, kulikuwa na vyama vya siasa vifuatavyo, Afro-Shiraz Party (ASP) kilianzishwa tarehe 5 Februari 1957, Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP) kilianzishwa mwaka 1959, Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kilianzishwa mwaka 1955 na Chama cha Umma kilianzishwa mwaka 1962. Vyama hivi vinadhihirisha kuwepo kwa mfumo wa demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa hata kabla ya uhuru. Tarehe 9 Desemba 1961 Tanganyika ilifanikiwa kupata uhuru wake kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza na hivyo kuendelea na mfumo wa demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa baada ya uhuru, ambapo mfumo huo ulitamkwa katika Katiba ya Uhuru (Independent Constitution of 1961). Tarehe 9 Desemba 1962 Tanganyika ilipata Katiba Mpya, ambayo iliitangaza Tanganyika kuwa Jamhuri.
Tarehe 12 Januari 1964, chama cha siasa Afro-Shiraz Party (ASP), kikiongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume, kiliongoza wananchi wa Zanzibar kufanya Mapinduzi na kuunda Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya Mapinduzi Vyama vya Siasa vingine pamoja na asasi za kiraia vilipigwa marufuku.
Tarehe 26 Aprili 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuwa nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano huo wa nchi mbili, umedumu kwa miaka zaidi ya hamsini, hivyo ni muungano pekee hai katika bara la Afrika. Hata hivyo, kuna changamoto kadhaa katika Muungano huo ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi na kupungua siku hadi siku.
Baada ya Muungano kulikuwa na Katiba ya Muda ya Muungano inayoitwa “The Interim Constitution of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar of 1964”, na mwaka 1965 ikatungwa Katiba Mpya ya Mpito inayoitwa “The Interim Constitution of Tanzania of 1965)”, iliyodumu hadi mwaka 1977. Katiba ya mwaka 1965 ilifuta mfumo wa vyama vingi vya siasa na kuanzisha mfumo wa chama kimoja cha siasa mwaka huo huo. Aidha, mwaka1967 lilitangazwa Azimio la Arusha ambalo liliweka misingi ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii katika mrengo wa ujamaa na kujitegemea na kuimarisha mfumo wa chama kimoja.
Mwaka 1977 vyama viwili vya siasa ASP na TANU viliungana na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM). Sambamba na hilo, ilitungwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 iliyoanza kutumika tarehe 26 Aprili 1977. Mwaka 1992, Serikali ya Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliunda Tume ya Rais ya Kukusanya Maoni Kuhusu Chama Kimoja au Vyama Vingi vya Siasa na kufanyika kwa Mabadiliko ya Nane ya Katiba yaliyorejesha mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania. Sababu za mfumo huo kurejea ni hizi zifuatazo:
a) vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa duniani, ambapo kulikuwa na msukumo wa nchi mbalimbali kutoka katika mfumo wa uchumi hodhi na siasa za kijamaa na kuelekea katika mfumo wa uchumi huria na demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa; na
b) msukumo wa ndani ya nchi wa kudai mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa, kutokana na hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwepo katika miaka ya themanini.
Baada ya mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa kurejea mwaka 1992, Vyama vya Siasa vimekuwa vikifanya jitihada za kutafuta wanachama, kunadi sera zao kupitia mikutano ya hadhara, kujiimarisha kitaasisi kupitia mikutano ya ndani na kuweka mifumo mbalimbali ya kiutawala. Hatimaye, vyama hivi vilianza kushiriki Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutafuta uongozi wa kisiasa. Tangu mwaka 1992 mpaka mwaka 2015 kulifanyika uchaguzi mkuu mara tano. Matokeo ya uchaguzi katika kipindi hicho yalionesha kukua kwa hali ya ushindani.
SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE YA MWAKA...
ZIJUE HAKI ZAKO DHIDI YA JESHI LA POLISI
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MH...
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Rip...
Ripoti Kuu Ya Mwaka Ya Mdhibiti Na Mkagu...
Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa H...