t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


Kigoma Ujiji Sexual Violence That Have Been Ignored By The Society.

 

Kigoma Ujiji – Sexual violence that have been ignored by the society.

Ukatili wa Kingono ndani ya kata ya Mwanga Kusini (Teleza)

Teleza ( ni jina lilipowe ubakaji unaotokea ndani ya kata ya Mwanga Kusini )

Jina hili lilitokana na kwamba, wakati wa usiku kuna wanaume wamekuwa wakiingia kwenye nyumba wanazoishi wanawake na kuwabaka. Watu hawa kabla ya kufika kwa mwanamke mlengwa huvua nguo zote na kubaki kama alivozaliwa, kisha wanajipaka grease ama mafuta ya kula mwili mzima. Baada ya hapo hubeba silaha aina ya kisu kikali ama mapanga, huvunja, ama hubomoa na kuingia kwenye nyumba anamoishi mwanamke kwa nia ya kubaka, kujeruhi, kuharibu mali na kuiba.

Suala hili linasemekana limeanza tangu mwaka 2016, ambapo wanawake kadhaa walipojeruhiwa na mmoja wa wanawake hao akaamua sasa lazima apaze sauti yake, ndipo wanawake wengi wakaanza kujitokeza juu ya suala hili.

Wakati wa kufanya shughuli za Uraghbishi suala hili lilijitokeza sana katika eneo la mwanga kusini, japo kwa jinsi lilivyoelezwa ni kama tukio hilo lilijitokeza na kuisha. Wakati wa mrejesho kwenye kata hata wakina mama waliotegemewa kuliongelea hawakuwa tayari kuliongelea na hivyo kuonekana kama tukio lililotokea muda mfupi na kuisha, baada ya Diwani kuingilia kati na baadhi ya watu kukamatwa.

Baada ya uraghbishi nilimfuata diwani ili aweze kunikutanisha na baadhi ya wahanga hawa. Knowing how sensitive the matter could be I wanted him to call anyone who can say anything about Teleza and not just those who were raped. Tulikubaliana aite wanawake as many as possible to try to find out how big the number is.

Lakini wanawake hawakujitokeza wengi sababu ya mvua lakini kwasababu wanawake wengi wameshaona haina maana sana kulizungumzia maana ni suala ambalo halina ufumbuzi. Kwa sabahu hii niliamua kuwafata wahanga wengine kwenye makazi yao baada ya kuongea na waliofika

Ramla na Sango (these are their real names and am sharing them with you privately)

Ramla and Sango were ready to speak about it. They said they want to speak as many times as possible and to the whole world if possible. They want the world to hear and know about what women are going through.

RAMLA

Ilikuwa ni siku chache baada ya kukorofishana na mume wangu, nikaamua kwenda kuishi kwenye nyumba yao. Siku ya tukio kulikuwa na msiba hapo jirani ambapo nilihudhuria na mada kuu kwa wanawake ilikuwa ni Teleza maana ndio ilikuwa imeanza kusikika kwa kasi sana (2016).

Usiku huo nikiwa nimelala, nikastukia mtu anainua net yangu, taa ikiwa imezimwa lakini akawa anamulika tochi kali usoni. Nilistuka sana, na sikujua cha kufanya maana akili ilinikumbusha kwamba hii ndio Teleza yenyewe sasa inanitokea. Alinikanya nisipige kelele na wakati huo akichezea visu vyake virefu mithili ya vile vya kukata nyama buchani. Niliogopa saana, lakini aliponisogelea nikashindwa kujizuia nikaamua kujitetea na kupiga kelele, hapo ndipo alianza kunipiga mapanga, na mengi yalipata mikono yangu miwili. Nilivuja sana damu na kuanza kupatwa na hofu kuu, kama watu hawatajitokeza na huyu jamaa akaendelea kunidhuru itakuwaje, na hapo nguo zangu alishazichana chana. Lakini naona majirani walisikia kelele zangu wakaanza kuongea na huyu mtu akakimbia. Na hapo ndo nilipata msaada. Nilivuja damu nyingi sana mpaka sasa picha ya hizo damu ikinijia, huwa ninastuka sana. Kadri damu ilivyozidi kuvuja ndivyo nilikuwa nasikia mwili wangu ukipata na baridi kali sana. Utashangaa mpaka sasa badiri hii haijawahi isha kila inapoingia usiku.

Tulienda police, nikaulizwa kama nilimtambua huyu mtu, nikasema sikumtambua. Basi wakaniambia nilipe elfu 5000 wakanipa PF3 na kuniambia kukiwepo na chochote cha ziada nitarudi niwaambie.

Nilienda hospitali, baada ya kupata matibabu nikarudi nyumbani, sikurudi tena Police kwasababu sikuona ninarudi kuwaambia nini tena, nilibaki na kazi ya kuuguza majeraha. Maana kama walikuwa na nia ya kulishuhgulikia suala hili walikuwa na sehemu ya kuanzia, kwasababu mimi sikuwa mtu wa kwanza kuripoti.  

Wifi yangu aliyekuwa ametoka Dar es Salaama kwa ajili ya msiba, akaamua kufuatili na kutaka wanawake wapaze sauti zao, lakini pia hatua za kisheria zichukuliwe. Aliita waandishi wa habari hawakuja, akamuomba mtendaji wa mtaa ashughulikie akaonekana kusita, ndipo alipomtafuta katibu wa mbunge ambaye yeye ndo aliita waandishi wa habari na hapo viongozi wa kata wakaanza kustuka na kujionesha wanashughulikia. WAnawake walioathirika na suala hilo walifika kama 40 kwa hesabu ya haraka haraka.

Kwangu mimi hili ni tukio la 2016 lakini mpaka sasa haya masuala bado yanaendelea. Na kama mwanamke hajaumizwa anaona hana sababu ya kupiga kelele wala kuhangaika kuripoti kwasababu haina maana, na hakuna msaada tunapata Zaidi ya watu kuja kukuona ili wakitoka hapo wakuite majina yao.

Na Zaidi wanawake wameona anapojeruhiwa bora aende akaripoti police ili aweze kupata matibabu, kwasababu hata kama umemtambua haisaidii, mtuhumiwa atakamatwa leo na baada ya siku kadhaa unakutana naye mtaani. Sasa usalama wako hapo unakuwa uko wapi? Police amekusaidia ama amekuweka hatarini Zaidi?

 

Mimi ninaona hili tukio, lengo lake kubwa ni kubaka na kumdhalilisha mwanamke, hayo mengine yanaongezeka kutokana na mazingira ya mtu. Sasa kama serikali imeweka sharia juu ya kumuingilia ndani kwanguvu na kwa lengo la kubaka, kwanini sharia ama police hawalichukulii suala hali Zaidi ya wizi ama kujeruhi?

Mimi kwangu hakuchukua kitu chochote, alikagua vitu vyote lakini hakuchukua kitu mle ndani.  Hii ilikuwa ni njia ya kunichafulia kwenye mtaa na nionekane Malaya tu.

Maeneo haya ambayo yamekuwa yakilalamikiwa, ni maeneo hatarishi, na hivyo kama police, ama viongozi wangeguswa saana wangehamishia nguvu zote huku. Haya matukio hayajawahi kuisha, yanaweza kupunguza spidi lakini bado yapo, ndiyo maana juzi kuna mwanafunzi pia ameingiliwa na kujeruhiwa. Na polisi wangekuwa na nia ya kweli, wangeshangazwa na wingi wa ripoti walizonazo juu ya suala hili.

Tangu siku siku hiyo na mwaka huo wa 2016, sipati usingizi wa Amani, kila wakati ninahisi kwamba kuna mtu ananifuata nyuma yangu,  ama kuna usiku ninakosa kabisa usingizi. Baada ya hilo tukio nililazimika kurudiana na mume wangu, lakini bado haijasaidia sana, kwani hata nikisikia panya kapita basi sitolala siku hiyo.  Tangu kipindi hicho sijawahi jisikia salama hata kidogo. Sasa hapo mimi nina mume, vipi wale wasiokuwa na mume?

Na wanawake wengi hapa tunaishi kwa wasi wasi sana. Kwasababu hata kama siku hiyo wamemkimbiza basi tunajua tu kwamba atarudi tu.

SANGO

Mimi haikuwa mara ya kwanza huyu mtu/ hawa watu kuingia kwangu. Kuna sehemu nilikuwa ninapanga mwanzo. Siku ya kwanza nikiwa nimelala, nilistukia kitasa kimedondoka, hivyo nilistuka nikapiga kelele na yeye akakimbia. Nikaona mazingira hayo si mazuri sana bora nihame. Nikatafuta nyumba nyingine nikahamia. Siku hiyo hiyo niliyohamia ndio siku aliniingilia tena, na siku hiyo nilikuwa nimechoka sana na shughuli zangu za kutwa nzima, hivyo nilistukia mtu yuko kitandani kwangu na ameshakata nguo zangu za ndani kwa kiwembe. Alinitishia kwa panga lakini mimi sikuogopa niliamua kupambana naye ndani na huku nikipiga kelele. Alipoona nakaribia kumzidi nguvu ndipo alinikata panga la kwenye mguu wangu, kisha akakimbia. Sikuweza kumfuata Zaidi maana nilikuwa uchi, lakini pia damu zilianza kutoka kwa wingi. Na kumbe kabla ya kuingia ndani aliacha amefungia majirani kwa nje na hivyo haikuwa rahisi kunipa msaada kwa haraka. Niliweza kuwasha taa,lakini nilistuka jinsi amavyo mapochi yangu yalikuwa yamepekuliwa. Nikakimbilia kuangalia pesa za mauzo yangu ya siku ya siku, ndipo nikagundua zimekwisha kuchukuliwa, pamoja na simu aliitolea betri na kuviweka mbalimbali, kulikuwa na tochi kubwa sana niliweka pembeni mwa kitanda, akawa imefunguliwa na kuondolewa betri zake na kutupwa sehemu mbalimbali. Hapo ndipo niligundua Zaidi kwamba huyu mtu alishaingia chumbani kwa muda mrefu kidogo kabla ya kutaka kutimiza lengo lake kuu.  Nahisi alikuwa na ujasiri huu wa kutumia muda mwingi chumbani kwani alijua si rahisi watu kutoka vyumbani mwao kwa haraka.

Nilienda police kama ambavyo wanawake wengine wanafanya kabla ya kupata matibabu, sikupewa msaada Zaidi ya kulipia PF3 kwa elfu 5000. Sikupewa msaada Zaidi police Zaidi ya police kustuka na kusema “Duh huyu TELEZA kakuumiza namna hiii? Alifanikiwa?’ Nikajibu hapana. Akauliza tena “hakunafanikiwa??”

Na bado nilipokwenda hospitali Dr naye ananiliuliza kama kama alifanikiwa, nilipojibu kwamba hakufanikiwa aliniambia “na nyinyi mmezidi sana kuwa wagumu mno ndio maana mnaingiliwa”

Kwangu mie picha niliyoondoka nayo pale ni kwamba yule TELEZA aliwaangusha, hakutimiza mategemeo yao. Yale maswali yao yalikuwa ni ya kejeli kabisa. Ndiyo, nilibaki na picha hiyo kwasababu nina uhakika mkubwa katika wanawake wote walioripoti hili suala kuna walioingiliwa, lakini waliwasaidia vipi Zaidi ya PF3 na dawa ambazo mtu ananunua mwenyewe?

Kana kwamba haitoshi baada ya hapo mimi hili suala liliniletea misuko suko sana mitaani, watu waliniita mie Malaya na wengine wakaenda mbali na kusema kwamba nilikula pesa za wanaume wanne na hivyo wakaamua kunifanyizia. Sokoni ninakouza bidhaa zangu nilionekana mtu wa ajabu, na watu hawakuisha kuninyooshea vidole. Nilikaa miezi mi tatu bila kwenda sokoni. Ilinichukua muda mrefu sana kujisafisha. Jamii inadharau sana mtu aliyeingiliwa na TELEZA.

Hata police aliyekuwa anashughulikia suala langu hili hakuniita kwa jina langu, aliniita mama wa TELEZA.

Mwanaume niliyekuwa na mahusiano naye alikuwa safari, lakini baada ya hili tukio hili tukio mahusiano yetu hayakurudi kuwa sawa na mwisho tulikuja kuachana. Alinilaumu kila siku kwamba niliwapanga wanaume mpaka nikashindwa kuwa mudu. Alinilaumu kwanini itokee kwangu tu.  Baba mkwe wangu alikuja kuniona baada ya wiki mbili kupita.

Suala hili lilitokea kwangu mwisho wa mwaka 2017, lakini mpaka mwaka jana bado kuna mtu alikuja na kuhangaika kutaka kuvunja komeo la mlango wangu, bahati nzuri baada ya tukio hili la pili, niliweka makomeo matatu, na cha kati nikakichimbia kwenye ukuta, hivyo mara hii alipokuja alihangaika saana kuvunja komeo lakini alishindwa. Alipoona ameshindwa akaamua kunifungia kwa nje.

Suala hili limepewa sura ya ushirikina, kutokana na kwamba mtu anakuja amepaka oil nyeusi sana mwili mzima na ukitaka kumkamata anateleza. Hii illipelekea hata hapo mwanzo watu walipokuwa wakiingiliwa hawakureport sana mpaka walipoanza kujeruhiwa. Na hata sasa ambapo watu wamekamatwa bado viongozi na vyombo vya usalama hawajalipatia uzito wa kutosha kwasababu bado wanasema kama sio ushirikina basi wasichana wanakuwa wamekubaliana nao, au wamekula pesa za wanaume wakakataa kulipa.

Mpaka kwenye mkutano mmoja wa hadhara wanawake walipolalamika, alitokea mzee mmoja na kusema kwamba, wanawake wanakuwa wamepatana nao, na kula pesa zao. Lakini bibi wa miaka kama sabini hivi akauliza na yeye anakuwa amekula pesa za nani mpaka asubiri kubakwa usiku?

Viongozi hawalipi uzito suala kwasababu linatokea kwa wanawake ambao hawaishi na wanaume.

Ndiyo maana ukienda police, wanachokuuliza ni Ulimtambua? Ukisema hapana na kesi inaishia hapo.

Lakini hili suala halitakiwi kuchukuliwa kishirikina wakati sisi wanawake ndiyo tunaendelea kuishi kwa hofu na kuumia. Tunatakiwa kusaidiwa. Kwamba mwanamke amesema hakumtambua haimaanishi kesi ndiyo iishie hapo. Kazi za wapelelezi ni nini?

Wakitolea mifano ya matukio mengine.

Wanaingia nyumba ambazo wanawake hawana wanaume. na wanakuwa wameshafatilia kuwa huyu mwanamke hana mwanaume humo ndani.

Kuna mwanamke mume wake alijilikana kuwa huwa anasafiri, lakini kumbe siku hiyo alirudi usiku. Katikati ya usiku huyo TELEZA akavunja mlango na kuingia, alipokuta mwanaume, alipanick na kukimbia. Pamoja na kwamba alikuwa na kisu na panga, alivitupa hapo chumbani na kukimbia.

TELEZA siku zote wanatabia ya kurudi na hawajaacha kurudi.

Mfano: Kuna mwanamke mtaani hapo hapo, alikuwa na mdogo wake ambaye alikuja hapo kwake baada ya kujifungua, lakini walimuingilia na kumbaka huyo mzazi, na kesho yake aliamua kurudi kijjini na katoto kadogo hivyohivyo. Lakini siku si nyingi walirudi tena kwenye hiyo nyumba, wakamkuta binti wa huyo mama mwenye nyumba waka mbaka. Yule binti alimtambua yule mbakaji maana alikuwa ana mtongoza siku si nyingi zimepita. Lakini utashangaa jinsi huyo mama alivyopata misukosuko kutoka kwa kiongozi wa mtaa.

Inaaminika wanatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume

Wanapoingia ndani, tiyari uume unakuwa umeshasimama.

Nyumba moja alikuwepo binti mmoja aliishi na mama yake, na alikuwa amepooza upande mmoja. Walimuingilia, na kumtumia mpaka nguvu zilipoisha ndipo yule TELEZa akaondoka. Na mara ya pili tena alimrudia na inasemekana alimuumiza sana huyu binti maana baada yah apo hali yake haikuwa nzuri. Hazikuisha siku nyingi sana yule binti alifariki.

Lengo ni kuweka lebal

“Na alama hii wanayotubandika ni alama tunayokaa nayo milele mpaka tunakufa.” Alisema Sango.

Na kwasababu waliona kwamba watu hawasemi. Mwanamke anakaa kimya ili kuficha aibu. Ndipo wakaanza kuja na mapanga na visu. Hata kama mtu hajafanya fujo, wakimaliza kumbaka wanaacha wamemkata na panga.

Kuna binti aliingiliwa mara tatu, na hakufanya vurugu, lakini mar azote tatu walimkata na kisu na kumuachia makovu kibao 

Kuna mama mtu mzima sana, na hakuwa na nguvu hata za kupambana nao, lakini bado waliamua kumkata mapanga

Hakuna response

Kuna msichana aliingiliwa na huyu TELEZA siku tatu mfululizo, na alimjua huyu jamaa. Akaenda akashitaki police lakini huyo kijana hajawahi kukamatwa mpaka leo.

Mtu huyo huyo, alitambuliwa sehemu nyingine na akashtakiwa, police walimkamata lakini baada ya siku akaachiwa.

Kuna dada mmoja anauza mama ntilie. Pale kwenye kijiwe chake, walikuja vijana wakawa wanasimuliana jinsi walivyoshindwa kutekeleza hazma yao ya kuingia kwenye nyumba ya mwanamke mmoja. Yule dada alimtambua yule alitaka kuingiliwa, na alipopita alimuuliza kama kuna watu walijaribu kuingia kwake. Yule mama kwa mshangao akakubali. Basi walienda kuripoti police, lakini police hawajawahi wakamata hao vijana, pamoja na Ushahidi huo.

Kijana mwingine alikimbizwa akiwa uchi, wakashindwa kumkamata. Lakini bahati nzuri wakakutana na nguo zake kwenye kichochoro. Walizitambua nguo hizi na walimkamata, wakampiga na kumfikisha police, lakini baada ya siku si nyingi alitoka. Yule aliyekuwa ameingiliwa, alipofuatilia Zaidi police walisema hasiwaingilie kwenye kazi yao, waache mtuhumiwa akauguze majeraha yake aliyopigwa na wananchi nyumbani

Hofu ya magonjwa na mimba zisizotarajiwa

Kuna mwanamke mume wake alikuwa amelala kwa mke mwingine. Aliingiliwa na TELEZA, hakusema kwa kuhofia kunyooshewa vidole na wanajamii. Baada ya siku chache akaanza kuumwa. Alipoenda hospitali ndipo wakakuta ana magonjwa ya zinaa na virusi vya ukimwi. Mwanaume wake alimwacha. Ndipo yule mama akaanza kusimulia alivyoingiliwa na TELEZA.

Kuna nyumba moja ambapo wadada walipanga hapo. Yule mwenye nyumba, aliwaingilia kwa zamu wale wa dada na huku akiwatishia kuwachinja endapo watapiga kelele. Mpaka siku mmoja msichana aligoma na kupiga kelele ndipo ilijulikana kwamba amekuwa akibaka wasichana wote. Na huyo baba alijulikana anaishi na virusi vya UKIMWI. Huyo baba mwenye nyumba alikimbilia Kigoma vijijini.

Jamii

Bado jamii mpaka sasa wanaliangalia suala hili kama kosa la mwanamke. Kwamba kila mwanamke ambaye haishi na mwanaume ni Malaya na anakuwa amejitakia kubakwa kwa kuwalia wanaume pesa zao. Na hii imepelekea hata viongozi am ahata police kutoshughulikia suala hili kwa nguvu na moyo wao wote kwa kuwa wameshavaa Imani kwamba wanaobakwa wote ni Malaya.

Kuna wakati kijana mmoja alikamatwa, alipohojiwa akasema kwama yule mwanamke ni hawara yake, ama kwamba alikuwa ni changudoa anajiuza.

Baada ya mazungumzo haya yaliyochukua masaa matatu (had to give them enough time till they emptied all they could say/ tell about TELEZA)

          I visited a 17 years girl, who is in form 3. While asking a lady who knew where this girl lives                with her family. She also narrated her own incident

Mwanzo nilipokuwa nikisikia masuala haya yakitokea, nilidhani ni masuala ambayo yanawatokea wasichana ambao wanajitakia, na kwamba labda muda mwingi wako kwenye vilabu vya pombe ama bar. Niliamini kabisa kwamba hawa wanawake wanajitakia masuala haya kutokea kwao. Nilihisi kabisa kwamba wanakula pesa zao na wanakataa kuzirejesha.,

Kamwe sikujua kwamba ipo siku yanaweza nitokea mimi hapa, na kwa jinsi ambavyo nilivyojijengea heshima yangu. Na wadhifa wangu nilio nao kama kiongozi sikuwahi kujjua kama vijana wanaweza nikosea adabu na kuniingilia nyumbani kwangu usiku na kunivua nguo na kutaka kunibaka.

Mimi nina nyumba imara kidogo  ukilinganisha na za wengine wengi. Sikusikia ni kwa namna gani huyu kijana aliingia. Sikusikia hata kidogo. Nilistuka kuna mtu anazunguka chumbani kwangu na nilipostuka tiyari suruali langu nililokuwa nimelala nalo lilishachanwa.

Nilivyo na umbile kubwa, nilijitahidi sana kupambana naye huyu kijana, na alipoona namzidi nguvu akatokoka na kukimbia. Hakunibaka na wala hakuweza kunijeruhi, lakini mimi naona alinidhalilisha vibaya sana, hasa pale nilipolazimika kusimama uchi mbele ya kijana kama huyu. Sikujua ni nani lakini pia sidhani kama ni mtu wa mbali. Hivyo basi watakuwa wanasimuliana juu yangu.

Imenifanya nijisikie vibaya sana maana jamii wanasema niliagana naye. Mie na heshima zangu ninaweza kuagana na mtu mwenye heshima pia, kwanini niagane na muhuni kisha niongee kwa watu.

Kwakuwa nilishasikia kuwa huwa wanarudi, nilisubiri kwa muda wa miezi bila kupata usingizi wa maana, maana nilijua wakati wowote atakuj.

          Now back to a 17 years girls of form 3

Tukio hili lilitokea mwaka jana niliwa form two. Tunaishi kwenye nyumba ya kupanga na tunapanga chumba na sebule. Tunaishi na mama yetu pekee, tukiwa watoto watano wa kike. Siku ya tukio, ndugu zangu wawili walikuwa wamekwenda kijijini. Na hapo tulikuwa na mgeni ambaye alikuja kututembelea akiwa na katoto ka kiume miaka kumi. Mtoto wa mama mkubwa.

Mtoto wa kiume huyu mwenye miaka kumi alilala kwenye kochi sebuleni. Sisi wasichana tulilala chumbani na mama yetu siku hiyo alienda kulala kwenye msiba hapo jirani.

Tukiwa tumelala usiku wa manane, hatukusikia kitu chochote, japo mdogo wetu wa kiume aliyekuwa sebuleni alisikia huyu kijana jinsi alivyovunja kioo cha kwenye dirisha na kufungua mlango. Kwa woga alijifanya amelala kwa woga.

Yule TELEZA alipingia ndani alienda moja kwa moja kwa yule mtoto kwenye kochi akamvua nguo na kumchunguza. Alipogundua kwamba ni wa kiume akamuacha ndo akaja chumbani kwetu.

Mimi binafsi sikumsikia akiingia chumbani bali nilimsikia akimlazimisha dada yetu (Mgeni) avue chupi na wakati huo huo akimtishia kwa panga. Ndipo na mimi nilistuka, na wadogo zangu wengine walistuka na kuanza kupiga kelele. Alitupiga kwa mapanga na mara nyingine alitukata kwa hilo panga lake. Tulizidi kulia kwa hofu maana tiyari tulishaumizwa sana. Alipoona hatunyamaxi akachukua mwiko mkubwa na kuanza kututandika nao. Wote tulikuwa tunajificha nyuma ya dada yetu ambaye aliumizwa Zaidi. Baba mwenye nyumba alisikia lakini walishindwa kutoka kwasababu walifungiwa nje pamoja na majirani wengine. Walianza kupiga simu kwa mama, na mpaka watu wanafika tiyari tulishaumizwa vibaya sana. Dada yetu alizimia.

Tulikimbizwa police na hatimaye kukimbizwa hospitali na kushonwa nyuzi tano tano kila mmoja wetu.

Tukio liliniogopesha sana. Lakini baada ya hapo jamii na shuleni ndio kuliniogopesha Zaidi. Nilitamani kuhama shule na nikamwambia mama yangu, lakini kwa kuwa hana uwezo na tiyari alishaingia gharama za kutufanyia matibabu ambayo ilibidi auze godoro moja ilibidi nivumilie tu. Shuleni wanafunzi walinitania saana kwa kuniita majina na kwamba mimi ni mke TELEZA. Lakini nilijikaza mpaka sasa wanaonekana wamesahau, labda mara moja moja mtu aamue tu kunichokoza kwa kuniita mke wa TELEZA.

Kwasasa siwezi kubeba kitu chochote kichwani kwani nilikatwa mapanga ya kichwani. Na dada yangu alimaliza mwezi mzima akivuja damu puani. Alivyopona aliondoka.

          Mama wa binti

Mimi biashara zangu ni kuuza dagaaa sokoni. Siku tukio limetokea sikuwa na pes ahata kidogo. Lakini ilibidi nikope kwa watu ili niweze kukodi tax itupeleke police ajili ya kupata PF3 kwa watoto 2 ilikuwa elfu 10,000. Kisha taxi hiyo ikatupeleka hospitali ambako walishonwa kwa elfu 30,000 kwa kila mtoto na kununua madawa kwa ajili ya matibabu. Hizi pesa hazikuwa kwenye mpango wangu na ilibidi niuze godoro la watoto ili niweze kulipa madeni ya matibabu.

Jamii bado walisema kwamba huyu TELEZA alikuwa ni bwana wangu kwa kuwa mimi sina mume alishafariki. Na wengine waliongeza kuwa nimekula pesa za hao vijana ndio maana wamewaingilia watoto wangu. Hii sentensi ilikuwa inanihuzunisha sana kwani nilihofia kama watoto wangu wataamini wataniona mimi ni mbaya. Nashukuru Mungu walielewa tu.

NA mtoto wangu wangu wa mwisho naona tangu siku hiyo amekuwa mgonjwa kabisa. Hayuko vizuri kiakili. Maana alishuhudia tukioa zima. Sasa amebaki na woga wa hali ya juu sana. Ikiingia jioni anaanza kujikunyata na kusikia baridi sana. Hayuko sawa kabisa

           Matukio wanayoyajua Zaidi

Kuna mama ameingiliwa mara tatu mpaka sasa na anabakwa mbele ya mtoto wake mdogo. Amechagua kutopiga kelele ili abaki akimlea na kumuhudumia mtoto wake bila kukatwa mapanga. Anasema kwamba yeye kwake ndiye baba na ndiye mama, akipigwa mapanga akalala ndani watoto watakula nini wakati huko police hakuna kitu wanakusaidia?

Kuna mwanamke mwingine amekuwa akiingiliwa, lakini pamoja na kutopiga kelele lakini bado huyu muhuni amekuwa akimuachia makovu. Ana makovu kila seehemu.

 

 

 

  

 

 

 

 

 

 


download REPORT Posted on : 15 May, 2019